Je, I´tikaaf inaisha kwa kuona Laylat-ul-Qadr?

Swali: Je, I´tikaaf inakatika pale ambapo mtu ataona alama ya Laylat-ul-Qadr kama kwa mfano mtu akaona usiku wa tarehe 25? Je, katika hali hiyo akate I´tikaaf yake?

Jibu: Asikate I´tikaaf yake. I´tikaaf imewekwa katika Shari´ah katika yale masiku kumi yote. Haijalishi kitu hata kama mtu ataona Laylat-ul-Qadr. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si alijua kuwa Laylat-ul-Qadr ni usiku wa tarehe 21 lakini pamoja na hivyo akaendelea I´tikaaf yake? Ndio, ilihali aliijua na kwamba imeshapita. Lakini hata hivyo alifanya I´tikaaf masiku yote kumi ya mwisho. Tunasema huenda I´tikaaf yako ikawa baada ya wewe kwishakuiona. Huenda ikawa katika manzilah ya Raatibah kwa faradhi. Kwa msemo mwingine ni kwamba anakamilisha thawabu za usiku. Kuna yeyote katika sisi awezaye kuthubutu kusema kwamba ameupa Laylat-ul-Qadr haki zake? Hakuna. Sote ni wapungufu. Tunamuomba Allaah atusalimishe kwa msamaha Wake.

Kwa hivyo I´tikaaf yako katika yale masiku yaliyobaki baada ya kuona Laylat-ul-Qadr – hapa ni pale ambapo kukisihi kweli kama umeona na kwamba mambo ndivyo yalivyo –  inakuwa katika manzilah ya Raatibah kwa faradhi. Unakamilisha thawabu. Hata kama umeona kweli endelea kufanya I´tikaaf. Unatakiwa kutoka lini? Utatoka pale litapozama jua katika ile siku ya mwisho ya Ramadhaan. Mwezi ukimalizika kwa siku thelathini, basi utatoka baada ya jua kuzama katika siku ya tarehe 31. Mwezi ukithibiti kuwa ni siku ishirini na tisa, basi pale utapothibiti wewe ndio unatoka. Iwapo tukadiria kuwa kuna mtu amekaa I´tikaaf na baada ya ´Ishaa ya usiku wa tarehe 30 ndipo kukatangazwa kwamba ndio siku ya kwanza ya mwezi, basi anatakiwa kwenda na asisubiri mpaka ataposwali swalah ya ´Iyd. Kwa sababu hapo wakati wa I´tikaaf utakuwa umeisha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa hafanyi I´tikaaf isipokuwa yale masiku kumi ya mwisho mpaka yaishe. Haya ni mambo huulizwa sana katia msikiti Mtakatifu. Utamkuta mtu ni miongoni mwa watu wa Jeddah au Twaaif na anatamani ule usiku wa ´Iyd kubaki na familia yake ambapo watu wanamwambia asubiri mpaka kupambazuke na waswali kwanza ´Iyd. Wameyatoa wapi haya? Ni lini I´tikaaf inaisha? Ni pale ambapo jua litazama katika ile siku ya mwisho ya Ramadhaan. Hapo I´tikaaf itakuwa imeisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/953
  • Imechapishwa: 10/11/2018