Je, inafaa kusoma kwa sauti ya juu katika swalah za kusoma kimyakimya?

Swali: Je, inafaa kusoma kwa sauti ya juu katika swalah za kusoma kimyakimya?

Jibu: Inafaa kusoma kwa sauti ya juu katika swalah za kusoma kimyakimya licha ya kwamba imechukizwa. Sunnah ni kusoma kimyakimya. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma kimyakimya katika swalah za kusoma kimyakimya na akisoma kwa sauti ya juu katika swalah za kusoma kwa sauti ya juu. Baadhi ya nyakati imependekezwa kusoma kwa sauti ndani ya swalah baadhi ya Aayah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya hivo. Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Abu Qataadah al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/123)
  • Imechapishwa: 22/10/2021