Je, inafaa kulala nikiwa na janaba?

Swali: Je, inafaa kulala nikiwa na janaba?

Jibu: Inafaa kwa mtu kulala akiwa na janaba. Isipokuwa kilicho bora ni mwenye janaba alale baada ya kuosha tupu yake na kutawadha wudhuu´ wa swalah. Hayo ni kutokana na yale waliyopokea watunzi wa vitabu sita kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye ameeleza:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anataka kulala ilihali yuko na janaba, basi huosha tupu yake na akatawadha wudhuu´ wake wa swalah.”

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (05/339) nr. (2309)
  • Imechapishwa: 05/06/2022