Je, inafaa kufunga masiku ya Tashriyq?

Swali: Je, inafaa kufunga masiku ya Tashriyq?

Jibu: Masiku ya Tashriyq ni yale masiku matatu baada ya ´Iyd-ul-Adhwhaa. Yameitwa hivo kwa sababu watu huning´iniza na kutandaza nyama juani. Lengo ni ili ikauke na isiharibike wanapoihifadhi. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu masiku haya matatu:

”Masiku ya Tashriyq ni masiku ya kula, kunywa na kumtaja Allaah (´Azza wa Jall).”

Mambo yakishakuwa hivo basi hayawi masiku ya kufunga. Kwa ajili hiyo amesema Ibn ´Umar na ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhum):

”Hairuhusu kwa mtu kufunga masiku ya Tahsriyq isipkuwa kwa ambaye amekosa dhabihu.”

Bi maana mtu anayefanya hajj ya Tamattu´ na Qiraan. Wanatakiwa kufunga siku tatu katika hajj na siku saba watakaporudi nyumbani. Hawa ndio wanaotakiwa kufunga masiku ya Tashriyq ili wasipitwe na msimu wa hajj ya kuyafunga. Hakuma mwingine anayeruhusiwa kuyafunga. Hata kama mtu anatakiwa kufunga miezi miwili mfululizo anatakiwa kuacha kufunga siku ya ´iyd na masiku matatu baada yake kisha aendelee na swawm yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.islamway.net/fatwa/8208/هل-يجوز-صيام-أيام-التشريق
  • Imechapishwa: 06/07/2022