Swali: Je, dhahabu za kujipamba ambazo zinavaliwa zinatolewa zakaah?
Jibu: Kwa mujibu wa maoni yenye nguvu ni kwamba dhahabu inayovaliwa inatolewa zakaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakuna mtu aliye na dhahabu au fedha na asiitolei zakaah isipokuwa siku ya Qiyaamah atapewa sahani za Moto zilizochochewa kwenye Moto wa Jahannam kisha apigwe nazo kwenye mbavu zake, paji lake la uso na kwenye mgongo wake. Kila zinapopoa zinatiwa moto tena kwa siku moja ambayo ni sawa na miaka 50.000 mpaka pale waja watakapohukumiwa. Kisha aone njia yake; ima kuelekea Peponi au kuelekea Motoni.”[1]
Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:
“Hakuna mtu aliye na dhahabu au fedha… ”
ni yenye kuenea na yamekusanya vito na vyenginevyo. Isitoshe ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa kuna mwanamke mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa pamoja na msichana wake ambaye mkononi mwake alikuwa amevaa bangili mbili nene za dhahabu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
“Unaitolea zakaah?” Akasema: “Hapana.” Akasema: “Utafurahia Allaah akikupa cheni mbili za Moto kwazo?” Akazitupa na kusema: “Nimezitoa kwa ajili ya Allaah na Mtume Wake.”[2]
[1] Muslim (987).
[2] Abu Daawuud (1563), at-Tirmidhiy (638) na an-Nasaa’iy (2479).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/154)
- Imechapishwa: 09/07/2026
Swali: Je, dhahabu za kujipamba ambazo zinavaliwa zinatolewa zakaah?
Jibu: Kwa mujibu wa maoni yenye nguvu ni kwamba dhahabu inayovaliwa inatolewa zakaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakuna mtu aliye na dhahabu au fedha na asiitolei zakaah isipokuwa siku ya Qiyaamah atapewa sahani za Moto zilizochochewa kwenye Moto wa Jahannam kisha apigwe nazo kwenye mbavu zake, paji lake la uso na kwenye mgongo wake. Kila zinapopoa zinatiwa moto tena kwa siku moja ambayo ni sawa na miaka 50.000 mpaka pale waja watakapohukumiwa. Kisha aone njia yake; ima kuelekea Peponi au kuelekea Motoni.”[1]
Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:
“Hakuna mtu aliye na dhahabu au fedha… ”
ni yenye kuenea na yamekusanya vito na vyenginevyo. Isitoshe ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa kuna mwanamke mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa pamoja na msichana wake ambaye mkononi mwake alikuwa amevaa bangili mbili nene za dhahabu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
“Unaitolea zakaah?” Akasema: “Hapana.” Akasema: “Utafurahia Allaah akikupa cheni mbili za Moto kwazo?” Akazitupa na kusema: “Nimezitoa kwa ajili ya Allaah na Mtume Wake.”[2]
[1] Muslim (987).
[2] Abu Daawuud (1563), at-Tirmidhiy (638) na an-Nasaa’iy (2479).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/154)
Imechapishwa: 09/07/2026
https://firqatunnajia.com/je-dhahabu-za-kujipamba-ambazo-zinavaliwa-zinatolewa-zakaah/