125. Allaah ana ukamilifu wa moja kwa moja

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Pamoja na hivyo Yeye (Subhaanah) hakuna kitu kinachofanana Naye; si katika dhati Yake, si katika majina na sifa Zake wala si katika matendo Yake. Kama ambavyo tunayakinisha kuwa Yeye (Subhaanah) anayo dhati ya kihakika na anayo matendo ya kihakika, basi vivyo hivyo anazo sifa za kihakika. Hakuna kitu kinachofanana Naye si katika dhati Yake, si katika sifa wala si katika matendo Yake. Allaah ni Mwenye kutakaswa kihakika kutokamana na yale yote yanayopelekea katika kasoro au uzukaji. Kwani Yeye (Subhaanah) ni Mwenye kustahiki ukamilifu wa moja kwa moja na haliwezekani Kwake jambo la kuzuka kwa sababu linapelekea kutokuwepo hapo awali na kuwepo muumba anayefanya liweze kuzuka na aidha kutokana na ulazima wa kuwepo Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa nafsi Yake.

MAELEZO

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anayo majina na sifa, viumbe pia wanayo majina na sifa. Lakini hakuna kufanana kati ya sifa za Allaah na sifa za viumbe Wake. Kama vile Allaah ana dhati isiyofanana na dhati za viumbe, basi vivyo hivyo majina na sifa Zake havifanani na majina na sifa za viumbe. Kwa sababu majina na sifa hufuata dhati inayosifiwa navyo. Basi kama dhati Yake hakuna anayejua jinsi yake isipokuwa Allaah, basi vivyo hivyo majina na sifa Zake hakuna anayejua jinsi yake isipokuwa Allaah. Kwa hiyo kuzungumzia kuhusu majina na sifa ni kama kuzungumzia kuhusu dhati.

Allaah (´Azza wa Jall) ametakasika na mapungufu yote. Upungufu ni kinyume cha ukamilifu. Allaah (Subhaanah) Ana ukamilifu wa moja kwa moja usioingiwa na kutoweka wala upungufu. Kuzuka

Kuzuka ni kupatikana kwa kitu baada ya kutokuwepo. Hili halistahiki kwa Allaah. Yeye kwa majina na sifa Zake ni wa milele, hakuna kitu kabla Yake. Kwa sababu kitu kipya kilichozuka  kinapelekea kwanza kuwa kilitanguliwa na kutokuwepo. Hakisemwi kitu ni kipya isipokuwa ikiwa kilitanguliwa na kutokuwepo. Pili ni kwamba kitu kilichozuka ni lazima kiwe na mwenye kukileta na kitendo lazima kiwe na mtendaji. Allaah (´Azza wa Jall) ametakasika na kutokuwepo na ametakasika na kuwa na mwanzo katika dhati Yake, majina na sifa Zake.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 211-212
  • Imechapishwa: 09/07/2026