Imaam Ahmad (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Allaah (Ta´ala) hatakiwi kusifiwa isipokuwa kwa yale aliyojisifia Mwenyewe au aliyomsifia kwayo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), pasi na kikomo wala mwisho:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[1]
Usifiaji hauwezi kufikia sifa Zake. Haitakiwi kuivuka Qur-aan na Hadiyth. Tunasema yale Aliyosema, tunamsifu vile Alivyojisifu na hatuyavuki. Tunaamini yale yote yaliyomo ndani ya Qur-aan; yaliyo wazi na yasiyokuwa wazi. Haturudishi nyuma chochote katika sifa Zake kwa sababu ya matusi ya wenye kutusi.”
Salaf wanamsifu Allaah kwa yale aliyojisifia Mwenyewe na kwa yale aliyomsifia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), pasi na kukengeusha, kukanusha, kumfanyia namna wala kumfananisha. Tunatambua kuwa yale ambayo Allaah amejisifu Mwenyewe ni haki, hakuna kitendawili wala mafumbo. Bali maaa yake inatambulika kutokana na muqtadha, na khaswa ikiwa yule mzungumzaji (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam) ndiye kiumbe aliye mjuzi zaidi wa kile anachokisema, mwenye ufaswaha zaidi katika kuibainisha elimu na mwenye kuwatakia viumbe mema zaidi katika kubainisha na utambulisho, kujulisha na kuongoza.
MAELEZO
Miongoni mwa maimamu waliotangulia ni Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah). Haya hapa juu ndiyo maneno yake. Allaah hasifiki isipokuwa kwa yale Aliyojisifia Mwenyewe au aliyomsifia nayo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haivukwi Qur-aan na Sunnah. Dalili zilizokuja kuhusu jambo hilo katika Qur-aan na Sunnah hazipotoshwi kutoka katika maana zake. Upotoshaji unakuwa sampuli mbili:
1 – Upotoshaji wa tamko kwa namna ya kwamba tamko likageuzwa kwa kuongeza au kwa kupunguza.
2 – Upotoshaji wa kimaana kwa namna ya kwamba tamko likafasiriwa kwa isiyokuwa maana yake sahihi.
Kufanya namna ni kupekua namna na jinsi zilivyo majina na sifa za Allaah. Kwa mfano mtu akauliza amelingana vipi, anasikia vipi, anaona vipi, atakuja vipi siku ya Qiyaamah na kadhalika.
Tunaamini kwamba yale ambayo Allaah amejisifia nayo yako juu ya uhakika wake, juu ya dhahiri yake na juu ya maana yake inayojulikana. Wala hatusemi kwamba hayako kinyume na dhahiri yake, kama wanavosema Mu´awwilah. Wala hatusemi kwamba hakuna yeyote anayejua maana yake isipokuwa Allaah, kama wanavyosema Mufawwidwah. Kwa sababu maana yake itakuwa kwamba Allaah ametuteremshia kitu ambacho hatujui maana yake. Hivyo kikawa ni mafumbo na vitendawili visivyojulikana. Allaah ametuamrisha kuzingatia Qur-aan yote:
كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُوْلُوا الْأَلْبَابِ
“Kitabu Tumekiteremsha kwako chenye baraka ili wapate kuzingatia kwa makini Aayah zake na ili wapate kukumbuka wale wenye akili.”[2]
Lau Qur-aan yote isingeeleweka maana yake, basi Allaah asingetuamrisha kuizingatia. Vipi atuamrishe kuzingatia kitu kisichojulikana maana yake? Hili haliwezekani kabisa. Basi maana za majina na sifa zinajulikana, lakini jinsi yake haijulikani kwetu. Ndiyo maana Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:
“Kulingana juu kunatambulika. Namna haitambuliki. Kuamini hivo ni wajibu. Ni kuuliza juu yake ni Bid´ah.”
[1] 42:11
[2] 38:29
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 208-211
- Imechapishwa: 09/07/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 208-211
Imechapishwa: 09/07/2026
https://firqatunnajia.com/124-qur-aan-yote-inafahamika/