Swali: Kuna baadhi ya watu wanapoumwa na mbwa au mbweha wanaenda kwa kabila fulani kwa ajili ya kunywa au kununua damu yao ili wapone. Wanatambua kuwa Allaah ndiye mponyaji lakini wanajengea hoja kwa kusema kwamba hakuna dawa nyingine inayofaa zaidi ya hiyo. Kuna mpaka mwanamke ambaye alitoa damu yake kwa lengo hilo. Wanasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakaribisha na kuwatukuza na akawaombea du´aa damu yao iwe tiba. Je, hayo ni sahihi?
Jibu: Haya si sahihi. Ni jambo linalotambulika kuwa wako watu wanaokunywa damu ya kabila fulani kwa lengo na kujitibu, lakini kitendo hicho hakijuzu kwa upande wa Shari´ah. Kwa sababu damu ni haramu kwa andiko wazi la Qur-aan. Allaah (Ta´ala) amesema:
حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ
”Mmeharamishiwa nyamafu na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa asiye Allaah.”[1]
قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ
“Sema: “Sipati katika yale niliyofunuliwa Wahy kwangu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu [mzoga] au damu inayomwagika au nyama ya nguruwe – kwani hiyo ni uchafu au ufasiki, kimetajiwa ghairi ya Allaah.”[2]
Ikiwa ni haramu basi ndani yake hakuna ponyo. Kwa sababu Allaah hakujaalia ponyo ya ummah huu katika vile alivyowaharamishia. Kwa ajili hiyo tunakemea jambo hili na tunasema kuwa ni jambo lisilokuwa na msingi wowote. Hivi sasa Allaah amejaalia kuwepo njia nyingi za matibabu na kusafisha damu. Wanaweza kwenda hospitali na kusafisha damu au kupata matibabu ya kung´atwa.
[1] 5:3
[2] 6:145
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/31-32)
- Imechapishwa: 09/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/31-32)
Imechapishwa: 09/07/2026
https://firqatunnajia.com/kunywa-damu-kwa-lengo-la-matibabu/