Swali: Jamaa´at-ut-Tabliygh wanasema kuwa wanalingania katika Uislamu kama jinsi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akilingania na wanatumia hoja Kauli Yake:

”Fikisheni kutoka kwangu ijapokuwa Aayah.”

Wanasema kwamba wanafanya yale aliyokuwa Mtume akifanya. Vipi mtu atajibu hilo?

Jibu: Ndio, ni sahihi ikiwa mnalingania katika Tawhiyd. Da´wah ya Mtume ilianza na Tawhiyd. Je, mnawafundisha watu Tawhiyd na kuwakataza Shirki? Katika hali hii mnafuata Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Lakini si kwamba mnaacha tu kulingania katika Tawhiyd. Zaidi ya hayo, mnazuia watu na hilo na mnawakimbiza na kuwatisha wale wanaolingania katika Tawhiyd. Hamfuati Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imeandikwa na: Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.ws/node/9914
  • Imechapishwa: 22/04/2015