Inawezekana kumuona Allaah usingizini

Swali: Maneno ya Shaykhl-ul-Islaam:

“Sifikirii kuwa kuna mtu mwenye akili ambaye anapinga kuonekana kwa Allaah (Ta´ala) usingizini.”

Nini anachokusudia kwa matamshi haya?

Jibu: Hayana neno. Kuonekana kwa Allaah usingizini ni jambo linawezekana, kama ilivyotajwa katika “al-Fataawaa” yake (Rahimahu Allaah). Kadhalika kama mfano wa Hadiyth:

“Nimemuona Mola wangu katika umbo zuri kabisa.”

Hata hivyo haipelekei kufananisha. Anaweza kusikia sauti, anaweza kuona nuru. Haipelekei katika kufananisha na akamfananisha na kadhaa na kadhaa. Kilichokatazwa ni kuona kikweli. Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” yake kwamba amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Tambueni ya kwamba hakuna yeyote katika nyinyi atakayemuona Mola Wake mpaka afe.”

Kwa maana ya kwamba kumuona kwa macho ya kichwa chake akiwa macho.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23785/هل-يمكن-روية-الله-تعالى-في-المنام
  • Imechapishwa: 27/04/2024