Inafaa kuzidisha idadi ya Dhikr zilizothibiti baada ya swalah?

Swali: Idadi ni kwa njia ya ki-´ibaadah au anaweza kuzidisha juu yake?

Jibu: Sunnah ni yeye afanye yale aliyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Baada ya hapo akiongeza haidhuru. Inafaa kwake kufanya maelfu. Lakini kwanza afanye idadi hii baada ya kila swalah kwa ajili ya kutendea kazi Sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23786/حكم-الزيادة-في-عدد-اذكار-الصلاة-على-الوارد
  • Imechapishwa: 27/04/2024