Anaanza kwa Istighfaar anapomaliza kuswali badala ya Takbiyr

Swali: Endapo imamu baada ya kutoa salamu atasema:

الله أكبر، الله أكبر

“Allaah ni mkubwa, Allaah ni mkubwa.”

kisha ndio akasema:

أستغفر الله

“Naomba msamaha kwa Allaah.”?

Jibu: Ataanza kwa:

أستغفر الله، أستغفر الله، أستغفر الله، اللهم أنت السلام، ومنك السلام، تباركت يا ذا الجلال والإكرام

”Namuomba Allaah msamaha. Namuomba Allaah msamaha. Namuomba Allaah msamaha. Ee Allaah! Hakika wewe ndiye as-Salaam. Amani inatoka Kwako. Umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”

Hivi ndivo alivokuwa akianza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Swali: Maneno yake katika Takbiyr?

Jibu: Takbiykr anakusudia:

سبحان الله

“Allaah ametakasika na mapungufu.”

Hadiyth zinafasiriana baadhi kwa nyengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23787/ما-الذي-يبدا-به-في-اذكار-الصلاة
  • Imechapishwa: 27/04/2024