Inajuzu kumfanyia Rukuu´ mzazi?

Swali: Je, inajuzu kumfanyia Rukuu´ yeyote kwa mfano wazazi wawili?

Jibu: Haijuzu, bali kufanya hivo ni shirki. Rukuu´ ni ´ibaadah anayofanyiwa Allaah kama mfano wa Sujuud. Hivyo haijuzu kumfanyia asiyekuwa Allaah.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/221-222)
  • Imechapishwa: 24/08/2020

Turn on/off menu