Inafaa kuwatii watawala wasiyohukumu kwa Shari´ah?

Swali: Utiifu kwa watawala ambao hawahukumu kwa Shari´ah ya Allaah ni wajibu na asli katika misingi ya Shari´ah ya Kiislamu? Au ni kwa ajili khofu kwao [kuwaogopa]?

Jibu: Ni wajibu kuwati kwa yale ambayo yana manufaa kwa watu unaoishi nao ilimradi hawajakuamrisha maasi na kukukataza na jambo la wajibu kwako. Kwa sababu kwa kufanya hivyo kuna utaratibu na amani na hivyo watu huepuka matatizo. Kwa kuwa kuwakhalifu na kuwaasi kunaleta matatizo kwako na kwa familia yako. Ama wakikuamrisha ufanye ya haramu au wakikukataza na jambo la wajibu katika dini usiwatii.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=129780
  • Imechapishwa: 08/04/2022