Inafaa kuuliza kama maiti alikuwa anaswali?

Swali: Ni yapi maoni yako imamu pindi anapoletewa mtu amswalie anaanza kuuliza kama alikuwa anaswali au haswali?

Jibu: Naonelea kuwa mtu asiulizie juu yake. Huku ni kupetuka mipaka katika dini na kitendo hicho kimeshabihiana na kupekua kasoro za waislamu. Kuuliza hivo ni Bid´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa anauliza juu ya mtu pamoja na kuwa wanafiki walikuwa wakati wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini hata hivyo hakuwa anauliza kama ni mnafiki au ni muumini. Ni kweli ya kwamba alikuwa anauliza kama mtu ana deni au hana deni kabla ya Allaah kumfungulia mali nyingi. Akiwa na deni ambalo hajalilipa alikuwa anasema:

“Mswalieni mwenzenu.”[1]

Baada ya Allaah kumfungulia mali nyingi akawa yeye ndiye ambaye anasimamia madeni ya watu.

Kuhusu yanayohusiana na dini na kuuliza juu ya maiti ni Bid´ah.

[1] al-Bukhaariy (2289).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/117)
  • Imechapishwa: 07/09/2021