Inafaa kukaa I´tikaaf mbali na kumi la mwisho la Ramadhaan?

Swali: Je, inafaa kukaa I´tikaaf katika wakati wowote mbali na lile kumi la mwisho la Ramadhaan?

Jibu: Ndio, inafaa kukaa I´tikaaf katika wakati wowote. Wakati wake bora zaidi ni katika zile siku kumi za mwisho za Ramadhaan kwa ajili ya kumwigiliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum). Imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa aliikaa I´tikaaf katika Shawwaal katika baadhi ya miaka.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (10/410) nr. (3810)
  • Imechapishwa: 23/04/2022