Ina maana kwamba mwanamke analipwa thawabu pungufu?

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Sijaona walio na akili punguani na dini pungufu wanaomghalibu mwanaume mwenye busara kama nyinyi [wanawake].”[1]

Je, inafahamisha kuwa malipo yake ni pungufu kutokana na hilo? Vinginevyo anakuwa ni mwenye kupewa udhuru?

Jibu: Sijui kitu juu ya hilo. Kwa sababu hilo ni jambo Allaah kamwandikia. Hakika mambo yalivyo ni kwamba hiyo ni sifa yake.

[1] al-Bukhaariy (306).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23534/هل-ناقصات-عقل-ودين-يعني-نقص-الاجر
  • Imechapishwa: 08/02/2024