Imamu kugeuza kuwa maamuma na kinyume chake

Swali: Imamu alikuwa anaswali na pambizoni mwake yuko maamuma. Akaja mtu wa tatu akamtanguliza mbele yule maamuma ambapo akawa imamu na imamu akawa maamuma na wakakamilisha swalah kwa hali hiyo. Ni ipi hukumu ya swalah yao?

Jibu: Katika hali hii maamuma akinuia kuwa imamu na imamu kuwa maamuma hakuna neno. Hali hii ni kama ambavo inafaa kwa imamu kugeuka kuwa maamuma ikiwa kuna haja ya kufanya hivo. Lakini haitakikani kwake kugeuza isipokuwa kutokana na haja inayopelekea kufanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 24/05/2021