Swali: Kipindi cha mwisho imekuwa ni jambo la kawaida pindi mtu anapokufa, basi wanafamilia wake wanachukua likizo kwa ajili ya kuwapokea wanaokuja kutoa tanzia katika jamaa na majirani. Zoezi hilo hufanyika kwa muda wa siku tatu. Katika siku ya kwanza huchinjwa kichinjwa na wakapelekewa wafiwa ikiwa imepikwa. Kisha baada ya hapo majirani na jamaa huchinja kichinjwa na kuwapa wafiwa kwa ajili ya kuwasahilishia msiba waliopata. Tulikuwa tunaomba kupata majibu juu ya maswali yafuatayo:

1- Ni ipi hukumu ya kukaa kwa ajili ya tanzia kwa njia kama hii?

2- Ni upi hukumu ya vichinjwa hivi vinavyozunguka kati ya majirani na jamaa?

3- Huku kwetu wanafamilia wa maiti daima husimama upande wa kulia kwa imamu wakati wa kuswali swalah ya jeneza. Ni ipi hukumu ya hilo?

4- Ni ipi hukumu ya kuliweka kaburi matofali ya bloki badala ya matofali ya udongo?

5- Ni ipi hukumu ya kuweka mataa makaburini kwa ajili ya zoezi la kuzika?

و السلام عليكم و رحمة الله و بركاته

Jibu:

بسم الله الرحمن الرحيم

و عليكم السلام و رحمة الله و بركاته

1- Kukaa chini kwa ajili ya kutoa pole ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah. Kwa sababu si Mtume (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah wake hawakufanya kitu kama hicho. Bali Jariyr bin ´Abdillaah al-Bajaliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Tulikuwa tukizingatia kukusanyika kwa familia ya maiti na kutengeneza chakula baada ya mazishi ni aina fulani ya kuomboleza.”[1]

an-Nawawiy amesema katika “al-Majmuu´”:

“Kuhusu kukaa kwa ajili ya tanzia, basi itambulike kuwa ash-Shaafi´iy, mtunzi na wenzetu wengine kwamba ni jambo lililochukizwa.”

Baya na khatari zaidi ni pale ambapo tanzia itaambatana na kuacha kazi na matumizi. Salaf hawakuwa wakiketi kwa ajili ya tanzia. Bali walikuwa wakiendelea na kazi zao na mambo yao ya kila siku. Ikiwa mtu atakutana nao katika wakati wowote wa mchana, wanawapa pole.

2- Nyama za vichinjwa hivi ni halali, lakini uchinjaji aina hii ni jambo la kizushi na lenye kukemewa. Salaf hawakuwa wakifanya hivo. Kubwa liwezalo kusemwa ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Watengeneezani familia ya Ja´far chakula! Kwani hakika wamefikwa na jambo lenye kuwashughulisha.”[2]

Hili lilifanywa katika ile siku ya kwnaza.

3- Sunnah katika swalah ya mkusanyiko ni imamu asimame peke yake katika safu. Asiweko yeyote atakayesimama pamoja naye isipokuwa kutokana na haja kama vile ufinyu wa msikiti.

4- Kuweka matofali ya udongo ndio bora kuliki matofali ya bloki kwa sababu matofali ya bloki yameguswa na moto. Wanazuoni wengi wamechukizwa na kitendo cha kuliwekea kaburi kitu chochote kilichoguswa na moto. Lakini kukiwa na haja ya matofali ya bloki kama kwa mfano matofali ya udongo yanavunguka na hayawi imara, basi katika hali hiyo itafaa matofali ya bloki kuchukua nafasi yake.

5- Hakuna neno kuangaza makaburini wakati wa kuzika, kwa sababu mataa hayo ni ya haja na si ya kudumu.

Muhammad bin Swaalih al-´Uthaymiyn ndiye ambaye ameandika majibu haya matano.

1414-10-08

[1] Ahmad (2/204) na Ibn Maajah (1612). ash-Shawkaaniy amesema:

”Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.” (Nayl-ul-Awtwaar)

[2] Ahmad (6/266), Abu Daawuud (3132) na at-Tirmidhiy (998) ambaye amesema Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/398-399)
  • Imechapishwa: 24/05/2021