Swali: Baadhi ya maimamu wanakokota Takbiyr kiasi cha kwamba hawasimami au kusujudu isipokuwa kwa kuchelewa jambo linalofanya baadhi ya maamuma kumtangulia. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Lililo bora ni kutoikokota Takbiyr ili kusipitike kile kilichotajwa katika swali. Takbiyr inatakiwa kutamkwa kwa ufupi ili kusipatikane kwa waswalaji kuchelewa kwa sababu ya uvutaji wa sauti ya imamu. Hivi ndio bora zaidi. Ikiwa kutapatikana kitu kwa waswalaji pasi na kukusudia, Allaah atasamehe hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf%2030-7-1434_01.mp3
  • Imechapishwa: 15/06/2020