Swali: Kuna kijana ambaye anatuswalisha umri wake ni miaka kumi na tano na kila siku anasoma ndani ya msahafu katika swalah zake zote…

al-Fawzaan: Ni swalah za faradhi?

Muulizaji: Ndio dhahiri.

Jibu: Hafai kuwa imamu. Huyu hastahiki kuwa imamu. Waweke mwingine. Ikiwa hawana mwingine asome kile atachoweza katika Suurah fupifupi na hakuna haja ya kusoma ndani ya msahafu katika swalah za faradhi. Hata za zilizopendekezwa bora zaidi ni kutosoma ndani ya msafu, tuseme juu ya swalah za faradhi?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-02-09.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014