Sunnah ni kuanza kukata swawm na tende

Swali: Mamangu anapenda kufutaru kwa maji ilihali kuna tende. Nimeshamnasihi kwa kumwambia kwamba Sunnah ni kuanza kufutaru kwa tende ikiwa zitapatikana. Akanambia kuwa anapenda kuanza kwa maji. Katika hilo kuna ubaya?

Jibu: Huku ni kwenda kinyume na Sunnah. Wajibu ni yeye kupenda yale anayopenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume alikuwa anapenda kuanza kufutaru kwa tende. Akiwa anataka ujira na thawabu basi aanze kufutaru kwa tende.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (16) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-03-07.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014