Imamu anamzungumzisha anayemteua kuwaswalisha wengine

Swali: Vipi ikiwa anayeteua mswaliji kuwaswalisha wengine ataongea wakati wa kumteua mtu?

Jibu: Hapana tatizo, kwani swalah yake imeshaharibika kuanzia pale ambapo alipopatwa na hadathi au alipokumbuka kuwa hayuko katika hali ya twahara. Kwa kuwa hayupo tena katika hali inayomruhusu kuswali, anaruhusiwa kuzungumza kwa kusema: “Simama, ee fulani uwaswalishe” au “Kamilisha swalah nao, ee fulani.” Anaweza pia kumpeleka mtu mbele kwa ishara ili awaswalishe, kwa sababu tayari amejua kuwa yeye si miongoni mwa watu wa kuswali katika hali hiyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24912/هل-تبطل-الصلاة-بكلام-من-استخلف-غيره
  • Imechapishwa: 03/01/2025