Imamu amekumbuka kuwa hana wudhuu´ kabla ya kumaliza swalah

Swali: Ikiwa mtu alikumbuka kwamba hayuko katika hali ya wudhuu´ kabla ya kutoa salamu?

Jibu: Dhahiri ni kwamba anapaswa kusimama na kumwambia mmoja wa waliopo: “Kamilisha swalah nao”, kwa sababu hajamaliza swalah yake na yeye anajua kuwa hayuko katika hali inayomruhusu kuswali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24911/حكم-الامام-اذا-ذكر-انه-محدث-قبل-التسليم
  • Imechapishwa: 03/01/2025