Imamu ambaye anachukiwa na maimamu

Swali: Tuko na imamu ambaye maamuma hawampendi na wanamchukia chuki isiyokubalika katika Shari´ah. Ni ipi hukumu ya kule kuwaswalisha kwake?

Jibu: Imepokelewa katika Hadiyth kuhusu watu aina tatu ambao swalah zao hazivuki masikio yao ambapo kumetajwa mtu ambaye anawaswalisha watu ilihali wanamchukia. Lakini inatakiwa kutazama kule kumchukia kwao; ikiwa wanamchukia kwa sababu ya dini yake kama vile upungufu wa dini yake, upungufu katika maadili yake, anachukulia wepesi mambo ya wajibu, anapuuza msikiti, anawafanya maamuma kugombana, hachungi wakati wake au anaenda mbio kufarikisha kati ya umoja wa waislamu, hiki ni kitu kinachopaswa kutazamwa. Atashtakiwa katika mamlaka husika katika wizara ya Waqf. Hapo watatenda kulingana na hali halisi na tatizo litakomeshwa. Lakini ikiwa ni kutokana na jambo lisilokuwa la sawa; mwenye nidhamu katika maadili na tabia yake, mwenye nidhamu katika ujio wake msikitini na hakuna neno juu yake na hakuna jingine wanachotaka isipokuwa ni kumhamisha kutoka katika kazi yake kwenda katika nyingine, haijuzu kwao kufanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-إمامة-الإمام-الذي-تكرهه-جماعته
  • Imechapishwa: 10/06/2022