Khaliyfah bin Khayyaat bin Khaliyfah bin Khayyaat; Imaam, Haafidhw na ´Allaamah wa kihistoria. Abu ´Amr al-´Usfuuriy, pia alikuwa akiitwa Shabaab. Mtunzi wa “at-Taariykh”, ””at-Twabaqaat” na vitabu vyengine.

Amemsikia baba yake, Ziyaad bin ´Abdillaah al-Bukkaa-iy, Sufyaan bin ´Uyaynah, Ismaa´iyl bin ´Ulayyah, Yahyaa al-Qattwaan, Ibn Mahdiy na wengineo.

al-Bukhaariy, Baqiyy bin Makhlad, ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan ad-Daarimiy, Abu Bakr bin Abiy ´Aaswim, Zakariyya as-Saajiy na wengineo wamehadithia kutoka kwake.

Alikuwa mwaminiwa, mtafiti wa koo. Ibn ´Adiyy amesema:

“Alikuwa mwaminiwa, mmoja katika wapokezi walio makini.”

Baadhi wamemfanya kuwa laini, lakini pasi na hoja.

Mutwayyin na wengineo wamesema: “Alifariki mwaka wa 240.”

Alikuwa na miaka 80. Amekosea yule ambaye amesema kuwa amefariki mwaka wa 146, kwa sababu babu yake alifariki mwaka wa 160.

Mwaka huohuo ndio alifariki Shabaab, akafariki Ahmad bin Abiy Duwaad, Abu Thawr, Faqiyh Ibraahiym bin Khaalid, Qutaybah bin Sa´iyd, Faqiyh Sahnuun na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (11/472-474)
  • Imechapishwa: 30/09/2020