Imaam Abul-Hasan al-Ash´ariy aliachana na Ahl-ul-Bid´ah na kujiunga na Ahl-us-Sunnah 1

Swali: Je, ni kweli kuwa Imaam Abul-Hasan al-Ash´ariy alijirejea kwenye madhehebu yake? Tunaomba utuwekee wazi hilo.

Jibu: Hili linapatikana katika vitabu viwili; kitabu chake “al-Ibaanah” na kimechapishwa na kutolewa. Vilevile yanapatikana kwenye kitabu chake “Maqaalaat al-Islaamiyyiyn”. Baada ya kutaja madhehebu mbali mbali, akaweka wazi kabisa ya kwamba yeye anaamini yale aliyokuwemo Imaam Ahmad bin Hanbal. Ameweka wazi hili na yanapatikana kwenye kitabu chake “al-Ibaanah” na kwenye kitabu chake “al-Maqaalaat”. Inasemekana vilevile kuwa yametajwa kwenye barua yake kwenda kwa watu wa Thaghr “. Haya yanapatikana kwenye vitabu vyake. Si kwamba yamenukuliwa kutoka kwake kimaneno. Bali yanapatikana kwenye vitabu vyake alivyoandika yeye kwa mkono wake. Hivi ni miongoni mwa vitabu vya mwisho alivyoandika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_03.mp3
  • Imechapishwa: 31/05/2015