Swali: Je, ni katika sifa maalum zinazomuhusu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kukaa chemba na mwanamke wa kando na kumtazama?

Jibu: Halina dalili. Kinachotambulika ni kwamba Haraam alikuwa ni Mahram yake kwa upande wa ujomba au unyonyaji, kama walivyoyabainisha hayo kikosi cha wanazuoni. Katika Hadiyth ya Rubay´a hakuna dalili ya kukaa chemba na kwamba kuna kitendo cha yeye kukaa naye chemba. Msingi ni kuenea mpaka kubainike jambo kwa dalili ya wazi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23849/%D9%87%D9%84-%D9%85%D9%86-%D8%AE%D8%B5%D8%A7%D9%89%D8%B5-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%8A%C2%A0%D8%A7%D9%84%D8%AE%D9%84%D9%88%D8%A9-%D8%A8%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%AC%D9%86%D8%A8%D9%8A%D8%A9
  • Imechapishwa: 19/05/2024