Swali: Je, kabla ya swalah ya Ijumaa kuna Sunnah ya Rawaatib Rak´ah nne?

Jibu: Ijumaa haina Raatibah kabla yake. Anachotakiwa ni mtu kuswali idadi atakavyoweza. Raatibah iko baada yake. Uchache wake ni Rak´ah mbili na wingi wake ni Rak´ah nne, au Rak´ah sita kutokana na baadhi ya mapokezi. Kuna salamu kila baada ya Rak´ah mbili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1431-08-08.MP3
  • Imechapishwa: 21/04/2015