Ibn ´Uthymiyn kuhusu kugusu tupu ya mtoto wakati wa kumtamba

Swali: Mwanamke mwenye wudhuu´ akigusa uchi wa mtoto wudhuu´ wake unachenguka?

Jibu: Wudhuu wa mwanamke hauchenguki akimgusa mtoto wake au akagusa dhakari yake au tupu yake. Kwa kuwa hilo halichengui wudhuu´. Hata kule mwanaume kugusa dhakari yake, hakuchengui wudhuu´ isipokuwa ikiwa ni kwa matamanio. Ama ikiwa ni bila ya matamanio, imependekezwa kutia wudhuu´ lakini sio wajibu.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (09 B)
  • Imechapishwa: 14/09/2020