Mwanamke kuwa imamu kuwaongoza wengine katika Tarawiyh

Swali: Je inajuzu kwa kikosi cha wanawake kuwa na imamu mwanamke akawaongoza katika swalah ya Tarawiyh?

Jibu: Inajuzu kwa wanawake kuswali pamoja katika mkusanyiko katika Tarawiyh na zile swalah tano. Mmoja wao awaongoze wengine katika swalah. Hili lifanyike katika moja ya majumba yao ambapo wametengwa na wanaume, kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimruhusu Umm Waraqah kuswali na wale wanaoeshi nyumbani kwake kuwa kama imamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Muntaqah min fataawaa Shaykh Swaalih bin Fawzaan (3/204)
  • Imechapishwa: 14/09/2020