Ibn ´Uthaymiyn mwanamke kuvaa suruwali nyumbani na nje ya nyumbani

Swali: Imeenea kati ya safu za wanawake kuvaa suruwali. Tumefikiwa na fatwa kutoka kwako na tumependa tujisikilie wenyewe kutoka kwako ili tufikishe kwa ujuzi. Ni ipi hukumu ya mwanamke kuvaa suruwali? Kuna tofauti kati ya suruwali pana na isiyokuwa pana? Hukumu hii ni nje ya nyumbani peke yake au imeenea mpaka nyumbani na sokoni?

Jibu: Naonelea kuwa mwanamke kuvaa suruwali ni haramu. Hilo ni kutokana na sababu mbili:

Ya kwanza: Sababu ya kwanza ni kujifananisha na wanaume. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wenye kujifananisha na wanaume.

Ya pili: Ni njia inayopelekea mwanamke kuvaa suruwali yenye kubana yenye kuonyesha umbile la mwili wake. Hata kama atadai kuwa yeye anavaa suruwali yenye pana, atafanya hivo kwa muda fulani halafu baadae atakuja kuvaa suruwali yenye kubana. Tukikadiria kuwa kuna mwanamke mwema anayeweza kufanya hivo, watamuiga wasiokuwa hivo. Hivyo ninachoonelea kuwa imekatazwa na kwamba haijuzu. Hili ni kwa ajili ya kufunga njia. Ikiwa haya ninayosema ni sahihi himdi zote ni za Allaah ambaye ameniwafikisha katika hilo na ikiwa si sawa ninamuomba Allaah anisamehe. Lakini pamoja na hivyo ni wajibu kwa mwanamke asiwe mfuata kichwa mchunga kila jipya linalozuka.

Mimi naitakidi kuwa mwanaume – ilihali ni mwanaume – lau atavaa suruwali atahisi aina fulani ya kushtuka kuwa imembana, kumuonyesha viungo na kadhalika. Vipi kwa mwili wa mwanamke? Hivyo mimi sionelei kufaa mwanamke kuvaa suruwali. Ni mamoja ikawa nyumbani wala nje ya nyumbani.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (25)
  • Imechapishwa: 16/01/2019