Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kuwavuta vijana kupitia mpira

Swali: Je, njia za ulinganizi ni lazima ziwe kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah au inaweza pia ikawa kwa njia ya mtu mwenyewe? Uislamu unasemaje juu ya Anaashiyd?

Jibu: Unakusudia nini njia na ulinganizi?

Muulizaji: Kama mfano wa Anaashiyd ni moja ya njia za ulinganizi ambapo zinaimbwa na vijana kwa ajili ya kuwaongoza wengine.

Jibu: Mtu anatakiwa kulingania katika dini ya Allaah kwa kutumia njia zote. Hata hivyo njia bora ni Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ

“Enyi watu! Hakika yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu na shifaa ya yale yote yaliyomo vifuani, na mwongozo na Rahmah kwa waumini.” (10:57)

Hili ndio bora zaidi.

Lakini vijana wakiwa mbali na tukataka kuwafungamanisha, na sio kwa sababu wenyewe kama wenyewe ni njia ya ulinganizi, ima kwa mazoezi yanayofaa au Anaashiyd zinazofaa, inafaa. Ikiwa inafaa kuwapa zakaah makafiri kwa ajili ya kuzilainisha nyoyo zao kuingia katika Uislamu. Inafaa kuwapa zakaah pamoja na mafukara kwa ajili ya kuwavutia kuingia katika Uislamu. Ulinganizi hauwi isipokuwa kwa Qur-aan na Sunnah lakini njia inaweza kuwa yoyote muda wa kuwa sio haramu. Wafungamanishe watu. Vijana wengi wanaweza kuwakimbia baadhi ya walinganizi kwa sababu si walaini kwao. Kwa hiyo ikiwa anataka kuwafungamanisha vijana kwa njia ya mfano wa kucheza mpira na kutoka baada ya ´Aswr, ni sawa kwa ajili ya kuwavuta kwake.

Swali: Je, Anaashiyd zimewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Siwezi kujbu swali hilo. Hivi sasa zimekuwa aina mbalimbali. Zimekuwa ni zenye kufanana na nyimbo zisizo na ladha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (224 B)
  • Imechapishwa: 02/10/2021