Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kuwaoa wanawake wa kinaswara na wa kiyahudi

Swali: Umetaja kwamba inajuzu kuwaoa kutoka kwa katika wanawake wa Ahl-ul-Kitaab. Je, mtu anaweza kuwasifu mayahudi na wakisto kwa wasifu huu moja kwa moja ya kwamba ni Ahl-ul-Kitaab kutokana na yale wanayofanya katika kukengeusha na kuviboresha vitabu vyao kila baada ya miaka kumi na kujinasibisha kwao kwa ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilihali amejitenga nao mbali?

Pili ni vipi mtu ataunganisha kati ya kuwaoa Ahl-ul-Kitaab ilihali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kusibaki dini mbili katika kisiwa cha kiarabu. Watoeni mayahudi na manaswara nje ya kisiwa cha kiarabu.”[1]

Naomba uniwekee wazi hilo?

Jibu: Miongoni mwa ya mwisho yaliyoteremka katika Qur-aan ni Suurah “al-Maaidah” mpaka wanachuoni wakafikia kusema kwamba Suurah “al-Maaidah” ndani yake hakuna chochote kilichofutwa. Ndani ya Suurah “al-Maaidah” kumehalalishwa kuwaoa wanawake wa Ahl-ul-Kitaab. Amesema (Ta´ala):

الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ

“Leo mmehalalishiwa vizuri na chakula cha Ahl-ul-Kitaab ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao na wanawake wenye kujichunga na machafu katika waumini wanawake na wanawake wenye kujichunga na machafu katika Ahl-ul-Kitaab kabla yenu.”[2]

Pamoja na kwamba Suurah hiyohiyo Allaah (Ta´ala) amesema:

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ

“Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu.”[3]

Wakristo wanasema kwamba Allaah ni moja ya utatu. Mayahudi wanasema kwamba al-´Uzayr ni mwana wa Allaah. Pamoja na haya Allaah amehalalisha wanawake wao. Ama kuhusiana na maneno yake:

“Hakika nitawatoa mayahudi na manaswara nje ya kisiwa cha kiarabu.”

Ni jambo linalofahamika kwamba mwanamke siku zote ni mwenye kumfuata mume wake. Hata kama yeye atabaki katika kisiwa cha kiarabu lakini yeye ni mwenye kufuata na si kwamba yuko peke yake. Kwa ajili hiyo iwapo mtu atamuoa mwanamke wa kinaswara katika mji wao na baadaye akamleta katika kisiwa cha kiarabu, ana haki ya kumbakiza. Kwa sababu anazingatiwa ni mwenye kufuata. Mpaka Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaita wake kuwa ni wasaidizi bi maana mateka au wafungwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mcheni Allaah juu ya wanawake. Kwani hakika wao ni mateka wenu.”

[1] al-Bukhaariy (3053), Muslim (163), Abu Daawuud (3029) na Ahmad (1691). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

[2] 05:05

[3] 05:73

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (55) http://binothaimeen.net/content/1260
  • Imechapishwa: 25/06/2020