Ibn ´Uthaymiyn aliyesahau Qur-aan baada ya kuhifadhi

Swali: Ni jambo linalojulikana kwamba wanafunzi wanakaririwa kitu kutoka katika Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall). Unapofika mwaka wa pili tunasahau baadhi ya Suurah tulizosoma mwaka uliopita klasini. Je, imeharamishwa kwa mtu kusahau baadhi ya Suurah hizi zilizokuwa zimethibiti?

Jibu: Itambulike kuwa pindi Allaah anapomneemesha mtu kuhifadhi kitu kutoka katika Qur-aan basi kwa hakika amemneemesha neema kubwa ambayo mtu hatakiwi kuifanyiwa mchezo. Kumepokelewa Hadiyth ambazo ndani yake kuna matishio makali juu ya yule mwenye kusahau kitu alichohifadhi kutoka katika Qur-aan. Lakini makusudio ni yule aliyesahau kwa kukipa mgongo na kukisusa. Ama kuhusu yule aliyekisahau kwa sababu ya kushughulishwa kutafuta maisha yake yeye na kwa ajili ya watoto wake na vilevile kushughulishwa na darsa zengine akiwa mtu huyu ni mwanafunzi, basi mtu hakuna dhambi juu yake. Kwa sababu hazingatiwi kuwa alikisahau kwa kukusudia. Allaah (Ta´ala) amesema:

رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Mola wetu usituchukulie tunaposahau au tukikosea.”[1]

Nataraji kutoka kwa Allah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwamba watu hawa hawatokuwa na madhambi. Lakini mimi nawashaji´isha wakichunge kile walichohifadhi kutoka katika Kitabu cha Allaah kama alivyoamrisha hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:

“Muwe na mazingatio juu ya namna mnavyohifadhi Qur-aan. Kwani naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake ni nyepesi zaidi kuponyoka kuliko ngamia wanaoachwa kujifungua wenyewe mikanda waliyofungwa.”

[1] 02:286

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1314
  • Imechapishwa: 30/06/2020