Ibn-ul-Qayyim matishio kwa wanaopinga kuonekana kwa Allaah Aakhirah

Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

Mlango: Makemeo kwa mwenye kukemea kuonekana kwa Allaah Aakhirah

Kumetangulia maneno Yake (Ta´ala):

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ

“Hapana! Hakika wao siku hiyo watawekewa kizuizi [wasimuone] Mola wao.” (83:15)

´Abdullaah bin al-Mubaarak amesema:

“Hakuna yeyote ambaye Allaah amemzuia [na kumuona huko Aakhirah] isipokuwa atamuadhibu.” Kisha akasoma maneno Yake (Ta´ala):

ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُو الْجَحِيمِ ثُمَّ يُقَالُ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ

“Kisha hakika wao bila shaka wataingizwa na waungue katika [Moto wa] al-Jahiym. Kisha itasemwa: “Haya ndio yale mliyokuwa mkiyakadhibisha.” (83:16-17)

Akasema:

“Kuhusu kuonekana.”

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 85
  • Imechapishwa: 27/08/2020