Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Enyi waumini wenye kuamini Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuweni na bidii [katika ´ibaadah] juu ya kumuona Allaah. Hii ni sifa kubwa ya kipekee ambayo ni kumuona Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).”

Mtu pindi anapomuona mwanachuoni mkubwa au kiongozi mwadilifu anahisi furaha kubwa. Vipi kuhusu kumuona Allaah (´Azza wa Jall)? Watu wanajisifu na kujigamba kwa kukutana na wakuu. Vipi kuhusu kumuona Allaah, ambaye ndiye Mola wa walimwengu (Subhaanahu wa Ta´ala)? Kwa ajili hii ndio maana wanashindana ili waweze kumuona na wanaogopa wasije kunyimwa kumuona Mola Wao (Tabaarak wa Ta´ala). Hivyo wanajiepusha na matendo ambayo yatafanya wakose radhi za Mola Wao. Wanajikurubisha kwa Allaah kwa yale matendo yatayowafikisha Peponi na kuweza kumuona Mola Wao (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 09
  • Imechapishwa: 27/08/2020