Ibn Taymiyyah amejuzisha Subha, lakini tunawafuata Salaf

Je, Salaf, baada ya kupatikana Subha, walikuwa wakiziweka mifukoni mwao, baada ya swalah kumalizika wanazitoa na kuhesabu Dhikr zilizowekwa katika Shari´ah? Au walikuwa wakihesabu Dhikr kwa vidole vyao? Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba hivi ndivyo walivyokuwa wakifanya. Subha ni katika Bid´ah za Suufiyyah. Inatosha. Mbali na kwamba Bid´ah hii inaenda kinyume na Sunnah, hatuonelei kuwa Ibn Taymiyyah (au wale walioafikiana naye) wamepatia kwa kujuzisha kuitumia. Yale ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametubainishia yanatosheleza; amesema na pia kuonyesha kuwa Dhikr inatakiwa kufanywa kutumia vidole vya mkono wa kulia.

Mpaka hii leo tunawaona namna ambavyo wale waislamu wa zamani wanawafuata kichwa mchunga manaswara. Subha msingi wake ni kutoka kwa manaswara[1] na zikawaingilia waislamu. Manaswara wameichukua kutoka kwa mabudha[2]. Kwa hiyo ni uzushi wa tangu hapo kale kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa dini kabla ya Uislamu. Ikawajia manaswara na wakaizua kama walivyozua utawa na mengineyo. Halafu ikatoka kwa manaswara na ikawajia waislamu. Sionelei kuwa inafaa kutumia Subha kwa kuwa inaenda kinyume na Sunnah Swahiyh.

[1] Tazama https://www.etsy.com/se-en/listing/222242983/crystal-anglican-rosary-or-protestant?ref=related-3

[2] Tazama http://www.buddhistmala.com/store/buddhist-prayer-beads.html

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (33)
  • Imechapishwa: 04/02/2017