29. Dalili ya kwamba unyayo wa Allaah ndio mguu Wake

29- ´Abdur-Rahmaan bin Muhammad al-Mahbuuriy amenihadithia: Ahmad bin ´Abdillaah bin Nu´aym amenihadithia: Haatim amenihadithia: Salamah amenihadithia: ´Abdur-Razzaaq amenihadithia: Ma´mar amenihadithia, kutoka kwa Hammaam bin Munabbih, kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kutatupwa Motoni na useme:

هَلْ مِن مَّزِيدٍ

“Hakuna zaidi?”[1]

mpaka Mola wa walimwengu aweke mguu Wake ndani ambapo utasema: “Tosha, tosha.”[2]

[1] 50:30

[2] al-Bukhaariy (4850), Muslim (2846) na Ibn Khuzaymah katika ”at-Tawhiyd”, uk. 97-98.

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 59
  • Imechapishwa: 04/02/2017