Ibn Baaz kuomba idhini mara tatu na kengele za kwenye milango ya nyumba

Swali: Leo inakuwa vigumu kuomba idhini mara tatu na inakuwa ni lazima kuzidisha khaswa katika yale majumba ambayo milango yake inakuwa mbali.

Jibu: Apige kitu kinachofikisha sauti kama vile kengele sambamba na kutoa salamu.

Swali: Je, azidishe mara tatu akijua kuwa hawakusikia?

Jibu: Sunnah ni kutoa salamu mara tatu. Lakini anaweza kupiga kengele au kitu kingine kinachofikisha sauti kwa sababu pengine hawajasikia sauti.

Swali: Kengele?

Jibu: Hapana vibaya, kwa sababu lengo ni kuzindua. Ni kama kengele ya saa na simu. Makusudio yake kwa kule kuitundika sio ya kabla ya kuja Uislamu.

Swali: Hakuwazuilii Malaika?

Jibu: Hapana vibaya – Allaah akitaka.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24246/حكم-الزيادة-على-السلام-ثلاثا-في-الاستىذان
  • Imechapishwa: 18/09/2024