Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
39 – Hakuna ambaye mguu wake utakuwa imara katika Uislamu isipokuwa kwa kujisalimisha. Yule mwenye kujipinda kuyajua yale asiyokuwa na elimu nayo na asikinaike na kujisalimisha, basi atakosa Tawhiyd takasifu, maarifa ya kweli na imani sahihi. Matokeo yake anakuwa mwenye kuyumbayumba kati ya ukafiri na imani, kusadikisha na kukadhibisha, kutambua na kukanusha. Atakuwa mwenye wasiwasi, mwenye kupotea na mwenye mashaka. Si muumini mwenye kusadikisha wala mwenye kukanusha na kukadhibisha.
40 – Imani ya mtu juu ya kuonekana [kwa Allaah] kwa watu wa Peponi haisihi ikiwa mtu atazingatia hilo kwa kupindisha maana. Kwa sababu kila maana, kukiwemo Kuonekana, ambayo inaegemezwa kwa Mola haitakiwi kupindishwa maana na badala yake mtu alazimiane na kujisalimisha. Hiyo ndio dini ya waislamu. Yule asiyeacha ukanushaji na ufananishaji, atapotea na wala hatopatia matakaso yoyote. Kwani hakika Mola wetu (Jalla wa ´Alaa) ni Mwenye kusifika kwa sifa za upweke. Hakuna kiumbe chochote kama Yeye.
MAELEZO
Imani ya kuamini Kuonekana haitosihi ikiwa mtu ataifanyia namna kwamba Allaah ataonekana namna fulani na hivyo akatumbukia katika kufananisha, kama alivosema Ibn Abiyl-´Izz. Wala haitakiwi kudai kuwa amefahamu tafsiri fulani inayoenda kinyume na udhahiri wake na ile maana wanayoifahamu waarabu wote.
Mu´tazilah na wengineo wanaomkanushia Allaah sifa na Kuonekana wanafanya hivo kwa madai kwamba wanamtakasa Allaah (Ta´ala) kutokana na kumfananisha. Fikira yao hiyo ni kosa, upindaji na upotevu. Ni vipi kufanya hivo itakuwa ni kumtakasa Allaah ilihali anamkanushia Allaah sifa zenye ukamilifu, kukiwemo sifa ya kumuona? Kwani kisichokuwepo ndio hakionekani. Ukamilifu ni kumthibitishia Allaah Kuonekana ambako kumethibiti ndani ya Qur-aan na Sunnah.
Mushabbihah wamepotea pale walipochupa mipaka katika kumthibitishia Allaah sifa kwa njia ya kwamba wakazifananisha sifa za Allaah na sifa za viumbe. Haki iko kati na kati. Sifa zinapaswa kuthibitishwa pasi na kufananisha, na mapungufu yanapaswa kukanushwa pasi na kumkanushia Allaah sifa. Ni uzuri uliyoje wa yale yaliyosemwa kwamba mwenye kumkanushia Allaah sifa anaabudia kisichokuwepo, na mwenye kumfanya Allaah kuwa na kiwiliwili analiabudia sanamu!
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 31-33
- Imechapishwa: 18/09/2024

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 31-33
Imechapishwa: 18/09/2024
https://firqatunnajia.com/18-visivyokuwepo-pekee-ndivo-havionekani/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)