Ibn Baaz kunyanyua mikono katika Takbiyr za swalah ya jeneza

Swali: Vipi kuhusu kunyanyua mikono katika Takbiyr za swalah ya jeneza?

Jibu: Bora ni kunyanyua, kama ilivyopokelewa kutoka kwa Ibn ´Abbaas na wengineo.

Swali: Je, kumepokelewa Hadiyth iliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Ipo Hadiyth aliyosimulia Ibn ´Umar ambayo imepokelewa na ad-Daaraqutwniy kwa cheni ya wapokezi nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22895/حكم-رفع-اليد-في-تكبيرات-الجنازة
  • Imechapishwa: 14/09/2023