Sayyid Qutwub amesema:

“Kuhusiana na kulingana juu ya ´Arshi, tunaweza kusema ya kwamba maana yake ni kama uangalizi juu ya ulimwengu huu. Dalili ya hilo ni kujua kwetu kwa yakini kutoka katika Qur-aan juu ya kwamba Allaah hawezi kubadilika. Hawezi kuwa katika hali ambapo hakulingana juu ya ´Arshi kisha ndio alingane juu ya ´Arshi. Tunaamini kulingana pasina kujua namna yake. Maneno Yake (Ta´ala):

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“… kisha akalingana juu ya ´Arshi.” (07:54)

isifasiriwe. Lililo bora ni kusema kuwa ni kinaya ya uangalizi. Ufasiri hapa hauendi kinyume na mfumo ambao tumeuashiria karibuni kwa sababu haukujengwa juu ya uamuzi na msimamo wetu wenyewe; umejengwa juu ya Qur-aan yenyewe na msimamo unaowakilishwa na Dhati na Sifa za Allaah (Subhaanah). Kwa uumbaji na ulinzi kuna vilevile elimu ilioenea…”[1]

Jibu: Yote haya ni maneno haribifu.

Swali: Hathibitishi kulingana [al-Istiwaa´]?

Ibn Baaz: Hapana, hapana. Ndio maana ya ulinzi. Hii ina maana ya kwamba anapinga kulingana ambako kunajulikana ni juu ya ´Arshi. Ni batili. Ni jambo lenye kuthibitisha kuwa alikuwa ni mjinga katika kufasiri Qur-aan.

[1] Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan (7/125).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=dWV4V3pxYrk
  • Imechapishwa: 26/08/2020