Ibn Baaz kuhusu maneno ya Sayyid Qutwub juu ya Mu´aawiyah na ´Arm bin al-´Aasw

Swali: Kuna maneno. Hatujui unasemaje juu yake. Mwenye nayo anasema:

“Mu´aawiyah na rafiki yake ´Amr hawakumshinda ´Aliy kwa kuwa walikuwa wajuzi zaidi kuliko yeye juu ya yale yaliyomo katika nafsi na si kwa sababu walikuwa na uzowefu zaidi kuliko yeye juu ya kutenda kwa njia inayonufaisha kwa wakati unaotakiwa. Walishinda kwa sababu walikuwa huru na hata hivyo wakajichukulia silaha wakati yeye [´Aliy] alikuwa amefungwa kwenye tabia yake ilipofikia wakati wa kuchagua silaha.

Kwa hivyo, Mu’aawiyah na rafiki yake ´Amr wakachukua uongo, udanganyifu, khiyana, unafiki na rushwa, ´Aliy hakuweza kuingia ndani ya shimo hili lirefu. Sio ajabu kuwa walifanikiwa na yeye akashindwa – huku ni kushindwa ambako kuko na cheo kuliko kushinda kote huku.” “Kutub wa Shakhswiyyaat”, uk. 242, cha Sayyid Qutwub.

Jibu: Ni maneno machafu. Ni maneno machafu. Ni kumtukana Mu´aawiyah na ni kumtukana ´Amr bin al-´Aasw. Ni maneno machafu. Ni maneno maovu. Mu´aawiyah na ´Amr walifanya Ijtihaad na wakakosea. Wakati Mujtahiduun wanaposea tunamuomba Allaah awasamehe wao na sisi.

Swali: Je, sio Takfiyr kuwatuhumu unafiki?

Jibu: Ni maneno ya kimakosa. Sio kufuru. Kuwatukana baadhi ya Maswahabah, au Swahabah mmoja, ni dhambi. Aliyezungumza hivo anatakiwa kutiwa adabu. Lakini akitukana wengi au kuonelea kuwa wengi walikuwa ni watenda madhambi, anaritadi kwa kuwa wao ndio wameifikisha Shari´ah. Akiwatukana ina maana ya kwamba ameitukana Shari´ah.

Swali: Je, vitabu kama hivi havistahiki kupigiwa marufuku?

Jibu: Vinatakiwa kuchanywa. Haya yanapatikana kwenye gazeti au?

Muulizaji: Yanapatikana kwenye kitabu.

Ibn Baaz: Ni kitabu cha nani?

Muulizaji: Sayyid Qutwub.

Ibn Baaz: Haya kweli ni maneno ya Sayyid Qutwub?

Muulizaji: Ndio, kweli kitabu chake “Kutub wa Shakhswiyyaat”.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=dWV4V3pxYrk
  • Imechapishwa: 26/08/2020