Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ikiwa kaburi liko katikati ya msikiti?

Jibu: Swalah haisihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah awalaani mayahudi na manaswara. Wameyafanya makaburi ya Mitume yao kuwa ni mahali pa kuswalia.”

Ukienda katika mji ambao misikiti yake iko na makaburi, basi usiswali ndani yake mpaka yafukuliwe. Isipokuwa ikiwa kaburi lilikuwa la kwanza na msikiti ukaja baadaye, katika hali hiyo msikiti unapaswa kubomolewa. Nchi ya kiislamu ina jukumu la kubomoa msikiti huo. Lakini ikiwa kaburi ndio jipya na msikiti ndio ulitangulia, basi katika hali hiyo ni lazima kulifukua kaburi na kulihamisha maeneo mengine.

Swali: Je, kuna uvuaji katika hali hii kuhusiana na kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hapana, hakuzikwa msikitini. Alizikwa nyumbani kwa ´Aaishah. Kosa lilifanywa na al-Waliyd wakati alipopanua msikiti ndipo chumba kikaingia ndani na hivyo ikawa ni shubuha kwa wachache wa elimu. Kwa hiyo lawama ni za kwa ambaye aliliingiza.

Swali: Je, airudie swalah yake ambaye ataswali ndani ya msikiti ambao uko na makaburi bila ya kujua?

Jibu: Ndio, airudie.

Swali: Mimi niliwahi kuswali miaka kadhaa ya nyuma pasi na kujua?

Jibu: Irudie.

Swali: Sijui ni swalah ngapi?

Jibu: Kulingana na dhana yako.

Swali: Vipi kuhusu kuzipangilia?

Jibu: Utazipangilia kila siku kwa hali yake kulingana na dhana yako.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24586/ما-حكم-الصلاة-اذا-كان-القبر-في-وسط-المسجد
  • Imechapishwa: 11/11/2024