Allaah amewanufaisha na kuwakusanya waislamu kupitia mfalme ´Abdul-´Aziyz, akainyanyua haki, akainusuru dini Yake na akaisimamisha kwaye jambo la kuamrisha mema na kukemea maovu. Amechangia kheri nyingi na neema nyingi ambazo hakuna anayezitambua isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall). Vivyo hivyo ndivo walivofanya watoto wake mpaka nchi hii ikawa ni kielelezo inapokuja katika Tawhiyd na kujitenga mbali na Bid´ah na ukhurafi.

Nchi hii ya Saudi Arabia ni nchi iliyobarikiwa na watawala wake wanapupia kutekeleza haki na uadilifu, kumsaidia mwenye kudhulumiwa na kumzuia mwenye kudhulumu, kueneza amani na kuzilinda mali na heshima za watu.

Kwa hivyo ni wajibu kusaidiana na watawala katika kuidhihirisha haki na kusambaratisha na kutokomeza batili mpaka kupatikane kheri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huquuq Wulaat-il-Amr ´alaal-Ummah Tarehe: 1417-04-29
  • Imechapishwa: 01/04/2024