Saudi Arabia haichukui msimamo mwingine isipokuwa kuwa dhidi ya Bid´ah na ukhurafi ndani ya dini ya Uislamu na uchupaji mipaka ambao amekataza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanazuoni, waislamu na watawala wa Saudi Arabia wanawaheshimu waislamu heshima kubwa. Wana mapenzi, upendo na matukuzo juu yao pasi na kujali wanatoka nchi au upande gani. Mambo yalivyo ni kwamba wanawakaripia watu wenye ´Aqiydah mbovu kutokana na yale wanayofanya katika Bid´ah, ukhurafi na sikukuu na sherehe zilizozuliwa ambazo hazikuamrishwa na Allaah wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu ni mambo yaliyozuliwa na kila kilichozuliwa ni Bid´ah. Waislamu wameamrishwa kufuata na sio kuzua kwa vile Uislamu umeshakamilika na hauna haja ya kitu kingine ambacho hakikuwekwa na Shari´ah na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wameipokea kwa kuikubali kutoka kwa Maswababah, wale waliowafuata kwa wema na wale wengine wote waliofuata mfumo wao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu Fataawaa wa Maqaalaat Mutanawwi´ah (1/229-230)
  • Imechapishwa: 01/04/2024