Ibn Baaz kuhusu Rak´ah mbili za msafiri anaporejea safarini

Swali: Leo misikiti mingi imefungwa. Je, aziswali nyumbani kwake?

Jibu: Udhahiri ni jambo zuri – Allaah akitaka. Ni vyema akiswali nyumbani. Kisichowezekana chote hakiachwi chote.

Swali: Je, si ni katika zile swalah zinazoswaliwa kutokana na sababu?

Jibu: Haidhihiri hivo, kwa sababu anaweza kuja amechelewa au kuja mapema. Anaweza kuchelewesha wakati wa ´Aswr mpaka Maghrib, na wakati wa Fajr akachelewesha mpaka jua lichomoze.

Swali: Rak´ah mbili hizo zinaswaliwa kabla hajaingia nyumbani?

Jibu: Ndio. Namna hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiukusudia msikiti kuswali kisha ndio anaketi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ajili ya watu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23980/ما-السنة-في-الركعتين-للقادم-من-السفر
  • Imechapishwa: 09/08/2024