Ibn Baaz kuhusu picha za kwenye magazeti

Swali: Picha za kwenye magazeti?

Jibu: Ni jambo linahitaji kuangaliwa vizuri, kwa sababu yamefungwa na hayatundikwi. Hata hivyo inatosha mtu akichukua tahadhari na akakata vichwa vyake, kwa sababu pengine ni vitabu ambavyo anavihitaji na magazeti ambayo wanazuoni wanayahitaji. Kwa hivyo kuna uwezekano yakajumuishwa na vile vitu vyenye kutwezwa au vitu vilivyofungwa ambavyo juu yake kuna kifuniko kingine. Kwa hivyo yafunikwe kwa makaratasi au kitambara kingine na yasiwe wazi. Kwa hivyo yasipokuwa wazi ni kama vile hayapo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24117/حكم-الصور-التي-في-المجلات
  • Imechapishwa: 31/08/2024