Haijuzu kumfukuza nyumbani

Swali: Je, inafaa kwa mume kumtoa nje mwanamke aliyeachika talaka rejea au ni lazima kwake kumbakiza na kumhudumikia?

Jibu: Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِن بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُجْنَ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ

”Msiwatowe katika nyumba zao na wala wao wasitoke isipokuwa wakileta uchafu wa wazi kabisa.”[1]

Haijuzu kwa mwanamke kufanya hivo. Wala haijuzu kwa mwanamme kumtoa nje ya nyumba.

[1] 65:01

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (39)
  • Imechapishwa: 31/08/2024